THIS IS DAR (HII NDIO DAR
MTUNZI MARCUSS99
Simu/ WhtsaWha 0757272749
Sponsored by Simulizi huru media
UTANGULIZI
Ukisikia ndugu yako anafanya kazi yupo Dar, au unataka kwenda kumtembelea, kabla ya kwenda muulize kwanza anafanya kazi gani,
Bila ya hivyo utageuzwa mtaji.
Au
Upo zako mkoa na unataka kuja DAR, jiandae na ukija ujue unakuja kufanya kitu gani, na ukishuka tu ubungo safisha macho yako
jiji Ni kubwa , watu Ni wengi pia kila mtu mjanja rafu ni nyingi.
Kama hauna sababu ya msingi ya kuja huku , wewe tulia tu .
Maisha popote unatusua .
Wakati wa mkoa wanakuja Dar , wakiamini Dar maisha Ni rahisi na kutusua pia ni rahisi , Wakati huo huo kuna wengine wapo Dar, na wanampamgo wa kurudi mikoani kwao, wakiamini labda mikoani maisha Ni rahisi
ZINGATIA .maisha Ni mchezo wa fikra, ukiwa na fikra Bora pia maisha yako yatakuwa bora
THIS IS DAR
SEASON ONE
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2017, natoka zangu shule, Airwing High school , nilishuka zangu pale kwa lulenge , mgongoni na begi langu nimechoka kiasi, kabla sijavuka upande wa pili wa barabara, niliona zogo , watu kibao wamejazana,
Nikajiuliza maswali, mengi,
"Pale Kuna mnada au Kuna mtu kafamaniwa , mbona zogo kubwa" nilijiuliza ,
Mwisho nikaona , sio mbaya ngoja kwanza nikachungulie.
Niliivuka ,barabara , taratibu kuelekea upande ule ambapo zogo lilikuwepo.
Nilipofika pale , nilimkuta kijana mmoja kawekwa chini , anapigwa makofi dabo dabo.
"Yaani utapeli wako Leo ndio umefika mwisho yaani Leo , pesa yangu unatoa na kifo utakiramba" alikuwa dada mmoja hivi , aliyevaa T-shirts ya Mpesa alisimama mbele ya Banda la Mpesa.
Bila ya Shaka yule alikuwa ni wakala ,
Maneno ya yule mdada ,yakanifanya nikae kwa makini zaidi na nivutike kuangalia na kutaka kujua Nini kimetokea.
"Tapeli? , ina maana huyu jamaa analeta utapeli , buza ? , au ni mgeni?" Nilijiuliza maswali mengi kuhusu yule jamaa , mengine nilipata majibu na mengine sikupata majibu.
Watu, waliendelea kumpiga na wengine walifika mbali na kutaka kumpiga tairi, hawa Ni wale waliochoshwa na vitendo vya wizi vilivyoshamiri pale Buza.
Kabla ya kumpiga tairi , kuna jamaa mmoja , ambaye anasemekana ni askari ambaye alikuwa na nguo za kiraia , jamaa alikuwa na moyo Safi sana,
"Jamani!, Jaman! , tulieni kwanza , kuchukua sheria mkononi Ni kosa kisheria na hata dini pia inakataza, kwahiyo Kama mutamchoma Moto , kwanza kabisa mungu atawahukumu na baada ya hapo Jamhuri itawashitaki" yule , Askari, alisema.
"Acha kumtetea huyo ni tapeli tu, huyo achana nae , mwache tumuue" Kijana , mmoja alisema , alikuwa kavua shati, mkononi ana bonge la jiwe utasema anataka kumuua tembo, kumbe anataka kumtwisha nalo mtu , kichwani.
"Naomba tumpe nafasi kwanza , ajieleze halafu baada ya hapo, ndio tutajua tunafanyaje" alisema , yule Askari.
Kwakuwa yule ni askari , na raia wote wanamjua Kama yule ni askari, iliwabidi kwanza watulie kidogo japo sio saaana.
"Kijana , unaitwa nani Ni mkazi wa wapi" yule Askari , alimuuliza yule kijana.
Wakati hayo yote yanaendelea Mimi ,nilikuwa nimesimama tu , nausoma mchezo tu , japo nilikuwa na njaa ,lakini taratibu njaa ilianza kukata.
"Naitwa , Hassan ,natokea Tanga, ila nimefikia kwa dada yangu , hapo Lumo mwisho, " alisema yule kijana huku machozi yakimtoka.
Anhaaa kumbe mgeni ,
Sasa na mgeni na utapeli wapi na wapi?
"Sasa kwanini unakuwa tapeli wakati ndio kwanza mgeni ,huoni unahatarisha maisha yako" yule Askari, alimuuliza .
"Ha..pana, hapana, Mimi sio tapeli" alikataa
"Wewe mshenzi nitakurukia wewe , wewe sio tapeli wewe ? wewe si umenitapeli hapa" yule mdada , alifoka kinoma, na hasira zake zilionekana wazi wazi.
"Wewe unamuhoji nini huyo, huyo ni tapeli , tuachie sisi" jamaa , mwingine nae alifoka Sana yaani utadhani yeye ndiye aliyetapeliwa kumbe alikuwa mpambe tu.
"Sasa sikieni , Kama mtu atampiga huyu jamaa ajue wazi kabisa Kama kesho ataamka akiwa kituo Cha Polisi, na wewe dada embu tulia upate haki yake, ukileta hasira hautapata pesa yako" yule , askari , aliwatisha wale raia wenye hasira Kali Kisha akamsihi yule mdada ,
"Enhee Hassani, wewe sio tapeli kivipi Wakati umekutwa na uthibitisho kabisa , embu jielezee hili utoke salama hapa, na hizo hela tunafanyaje kuzirudisha " yule Askari, alimuuliza yule jamaa.
Jamaa ,ikabidi aanze kuhadithia mwanzo Hadi mwisho.saa chache zilizopita . Alianza kuhadithia.
MASAA MAWILI YALIYOPITA.
Mimi naitwa , Hassani , Ni mkazi wa Tanga ,Dar hapa nimefikia kwa ndugu yangu tu , na tangia nifike hapa Nina siku tatu tu mpaka hii Leo,
Masaa matatu yaliyopita , Shemeji yangu , aliniagiza sokoni, akanambia nije huku Buza kwa lulenge , sababu huku bidhaa Ni nyingi na pia masoko Ni mengi.
Alinipandisha gari la Temeke - gongo la mboto , alinambia nimwambie konda anishushe Buza kwalulenge , na kweli nilimwambia , na kweli alinishusha.
Ile nashuka tu Buza kwa lulenge , nilisikia naitwa .
"Hassan ... , Hassan" kugeuka nyuma nilikutana na jamaa wawili , kiukweli sikuwajua , pia nilijiuliza wamenijuaje .
"Habari yako Hassan" walinipa mkono wote wawili, na Mimi niliipokea mikono yao.
"Najua hutufahamu, ila sisi tunakufahamu kiasi, wewe si Hassan ?, Umetoka Tanga juzi?, Umefikia kwa ndugu yako?" Kila walichoniuliza kilikuwa Cha kweli.
"Yeah ni kweli ,munachosema ila bado sijawajua na pia bado sijajua nyinyi Ni wakina Nani" niliwauliza.
Walikuwa vijana tu , masharobaro , wapo smart sana ,
"Usijali,embu tusogee pembeni kidogo tuongee vizuri, Bwana Hassan" waliniambia , sikuweza kubisha, sijui Ni Nini kilinikuta , lakini nilijikuta nawafata tu.
Tulisogea pembeni kidogo tu ambapo hapakuwa na msongamano wa watu wengi.
"Bwana Hassan, Sisi Ni Freemason na lengo letu kubwa Ni kukubadilishia maisha yako, tumetumwa kutoka makao makumuu ya Freemason, tuje tukufatilie sababu inaonesha nyota yako inang'aa Sana" alinambia jamaa mmoja ,
nilistuka."Heee! Freemason ?"
"Usiogope Hassan, haKuna kafara ya damu ambayo itatakiwa, Wala hautaambiwa uuwe mtu , ila Kuna masharti kidogo tu , itabidi uyafanye , kabla hujaingia, je upo tayari , maisha yako yatabadilika " aliniuliza Yule mwenzie.
"Sawa Kama hautoi damu, haina shida na je masharti yapi hayo, "
Niliwauliza, kiukweli maisha mazuri niliyatamani, na ukizingatia nilikuwa sina mbele wala nyuma.
Walitizamana usoni , Kisha wakanambia , "inabidi utoe laki nne na elfu tisini na tisa "
Nilistuka , kidogo , kiukweli kujiunga nilitaka sababu waliniahidi maisha Safi lakini pia ,sikuwa na pesa.
"Daah Sasa mbona hapa sina hela ndugu zangu"niliwaambia.
Walicheka Kisha wakatizamana usoni.
"Usijali , naomba utujibu , je upo tayari kwa lolote tutakalo kwambia Kama sehemu ya masharti, pia tunakuahidi ukishatimiza masharti hayo tu , Leo Leo tunaenda makao makuu, sisi na wewe unaapishwa halafu unapewa gari na nyumba" waliniambia.
"Ndiyo nipo tayari " niliwajibu.
"Safi sana umesema hapo hela hauna" waliniuliza.
"Ndiyo," niliwajibu.
"Sawa usijali, chukua hii hirizi to mfukoni halafu nenda pale kwa wakala mwambie atume pesa Katika namba hii 075****** , jina Rashidi Mrisho , wakati yeye anatuma pesa wewe ingiza mkono mfukoni halafu fanya Kama unakibinya binya hivi ,Yule wakala atasahau kukwambia umpe hela , na ukishamaliza Rudi hapa ".waliniambia. walinipa ile hirizi.
"Sawa, niliitikia" niliipokea
Na kwakuwa na Mimi nilikuwa na kile kihirizi , nilijiamini Sana.
Nilipiga hatua Hadi kwa wakala.
Hadi nafika kwa wakala nilikuwa nawaona
Nilimkuta wakala anachezea simu yake ,
"Dada habari " nilimsalimia
"Salama , karibu "
"Natak kutuma , hela voda " nilimwambia
"Shngap" aliniuliza.
"Laki nne na tisini na tisa" nilimjibu.
Basi , Yule mdada akanambia nimtajie namba , na Mimi nikamtajia.
Wakati hayo yanaendelea, nilikuwa bado nakibinya binya kile kihirizi , nikitarajia atasahau
"Jina Rashidi Mrisho" aliniuliza.
"Ndiyo dada ," nilimjibu huku nikiendelea kukibinya tu.
"Haya ,tayari Kaka nishamaliza kutuma , nimetuma laki nne na tisini na tisa , haya naomba hela " alinambia Yule dada.
Nilistuka , sasa mbona kakumbuka, kuangalia nyuma walipokuwa wamekaa wale jamaa , sikuwaona tena
"Wewe Kaka naomba hela yangu" wakala alibwata kwa sauti ya juu
Kwakuwa sikuwa na hela Nilijing'ata ng'ta , Mara Wakala akaanza kunipigia kelele za mwizi
Dakika mbili watu walijaa, wamenipiga Sana.
JAMAA , ALIMALIZA KUHADITHIA HUKU ANALIA.
"Basi sawa , jamani mumesikia ?, Kumbe Hassan Yeye mwenyewe kaibiwa " alisema Yule Askari.
"Atajua mwenyewe hii ndiyo Dar. atajua mwenyewe, Mimi nataka hela yangu" wakala alifoka
"Sawa , Japo umeibiwa ,ila itabidi ulipe hela ya watu, kwanza tunamba simu yako, halafu tupe namba za ndugu zako ili walipe hili deni " yule Askari , alisema.
Jamaa , alitoa simu yake , ilikuwa Tecno Y3 , pia alitaja namba za ndugu zake ,
Na walipigiwa na walisema wanakuja.
Mpaka pale, nikavaa begi, langu nikaondoka zangu, sikushuhudia kilichoendelea lakini nilisikia kama ndugu zake walikuja na walilipa.
DAR USIPOKUWA MAKINI , UNAWEZA KUGEUZWA MTAJI.
**********MWISHO*************
0 Comments